WASIFU WA MWALIMU
•
Tangazo la biashara: Ahadi kwamba atapunguza
kilo 11 katika majuma mawili kwa kutumia kitu kilichokuwa kinatangazwa.
– Chumvi
nyingi ilikuwa imeongezwa: alipunguza siyo zaidi ya nusu kilo.
•
Watabiri wa hali ya hewa walitangaza kuwa kesho
yake ingekuwa siku ya jua na joto mwisho wa mwezi wa nne (Aprili).
– Pilipili
ilikuwa imeongezwa: kesho yake kukawa na mawingu, radi na mvua kubwa ya mawe.
•
Yule jamaa aliyekuja kukuuzia ile simu pale
kwenye stendi ya basi; alikuuzia kwa nusu ya bei halisi ya ile simu.
– Huyu
alikuwa amechanganya chumvi na pilipili na chloroquine: Alikuwa ameiiba simu hiyo
kwa abiria mwingine kama wewe muda mfupi kabla.
Hivyo ndivyo sifa za watu zinavyotangazwa na kuwekwa mbele
za jamii ya wakazi wa dunia. Kuna chumvi nyingi, pilipili na hata sumu
zinazochanganywa ndani yake. Ukweli wenyewe hauelezwi, na uongo mwingi hutangulizwa!
•
Wengi wanasemwa katika hali ambayo si ya kweli
(too good to be true)! Na bado ulimwengu unanunua taarifa hizo na
kuzishangilia.
•
Mwalimu wa kweli hatangazwi na kile watu
wasemacho kumhusu, bali kwa yale aliyoyatenda, anayoyatenda na atakayotatenda!
Wasifu wake unajiuza; “chema chajiuza, kibaya chajitembeza”
•
Mwalimu Mwenye Ukweli Halisi anajiuza kwa kazi
zake za thamani kuu!!!
WASIFU WA MWALIMU
•
JE, YEYE ALIKUWA NANI?
•
YEYE NI NANI?
•
ALIFANYA NINI?
•
ANAFANYA NINI?
•
ATAFANYA NINI?
•
WASIFU WAKE UNAKUHUSUJE?
•
YEYE ALIKUWA NANI NA NI NANI SASA?
Yohana 1:1-3, 14 “Hapo mwanzo kulikuwako Neno,
naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. Huyo mwanzo alikuwako
kwa Mungu. Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote
kilichofanyika…. Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu;
nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba;
amejaa neema na kweli.”
•
1 Yohana 5:8: “Kwa maana wako watatu washuhudiao
mbinguni, Baba, na Neno, na Roho Mtakatifu, na watatu hawa ni umoja.”
•
ALIKUWAKO KWA MUNGU, NAYE ALIKUWA MUNGU:
•
Yohana
8:58 “Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambia, Yeye Ibrahimu asijakuwako, mimi
niko.”
•
Waebrania 1:1,2 Mungu, ambaye alisema zamani na
baba zetu katika manabii kwa sehemu nyingi na kwa njia nyingi, mwisho wa siku
hizi amesema na sisi katika Mwana, aliyemweka kuwa mrithi wa yote, tena kwa
yeye aliufanya ulimwengu.
•
Mwanzo 1:26
“Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu…”
•
Kumbukumbu
la Torati 6:4 “Sikiza, Ee Israeli; Bwana, Mungu wetu, Bwana ndiye mmoja.”
•
Yohana
10:30 “Mimi na Baba tu umoja.”
•
CHEO “MWANA” KILIANZIA WAPI?





